Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akicheza ngoma ya asili ya Mkoa wa Kagera wakati alipokuwa akilakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella .
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella akimkabidhi Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing Hati na ramani eneo lililotengwa na serikali ya mkoa kwa ajili ya kujenga chuo cha Ufundi (VETA) cha Kitaifa kilichoahidiwa na serikali ya China wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo mwaka jana.
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akipokea zawadi ya ramani ya Afrika Mashari iliyochorwa kutoka kwa wanafunzi wa shule ya Mgeza Mseto.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Aise Bukoba pazuri saaaaaaaaaaaana!! Karibuni ambao hamjawahi kufika huko!!
ReplyDeleteHicho chuo cha Veta kikijengwa kitainua mkoa huo ambao uko pembezoni lakini una mandhari nzuri hasa maeneo yanayopakana na ziwa viktoria. Walio na uwezo wa kuwekeza nao wafikirie kufanya hivyo ili mkoa uendelee mbele.
ReplyDeletesafari hii hajavishwa kofia ya ccm?
ReplyDeleteUkitaka vya uvunguni sharti uiname.Wachina wanajua nini wanataka, ndiyo maana babu balozi anakatika na midundo ya kina waitu.
ReplyDeleteUkiangalia majengo mazuri pale mjini katikati yaliyochukuliwa na shirika la nyumba yameandikwa kwamba yalijengwa mwaka 1956, hii inaonyesha utaifishaji usingesababisha uzorotaji wa kuendeleza miji mikoa ingekuwa imejengeka sana. Fursa zipo za kuendeleza miji hata watu binafsi wathubutu kuwekeza majengo ya vitega uchumi kuendeleza mikoani na wilayani
ReplyDelete