Benki ya NMB jana ilikabidhi pikipiki 5 aina ya Honda kwa jeshi la polisi kwaajili ya kusaidia kazi za kila siku za jeshi hilo katika hafla iliyofanyika nje ya ukumbi wa St. Gasper katika mkutano wa maafisa wa polisi unaoendelea mjini hapa.

Pikipiki hizo zilizokabidhiwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh Mathias Chikawe na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Borgols, zina thamani ya shilingi Milioni 10.

Waziri Chikawe alishukuru NMB kwa kuona umuhimu wa kusaidia jeshi la polisi na hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo. “ Tunashukuru sana kwa hizi pikipiki, zitatusaidia sana kuboresha utendaji wa polisi, tutaendelea kuwa wadau wenu muhimu,” aliongeza Mh Chikawe.

Team ya NMB ipo Dodoma kwenye mkutano wa maofisa wa Polisi na kuonesha kuwa inawajali katika kipindi cha mkutano, NMB ina mabanda kadhaa ya maonyesho nje ya ukumbi wa St Gasper huku wakitoa huduma mbalimbali kama kutoa na kuweka fedha kupitia huduma ya NMB Wakala huduma mpya inayoshirikisha mawakala wa MaxiMalipo, Kufungua akaunti kupitia Chap Chap Instant Account pamoja na elimu kwa ujumla juu ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Boghols akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani,Mathias Chikawe ufunguo wa pikipiki ambazo NMB imetoa kwa jeshi la polisi kwaajili ya kurahisisha kazi zao za kila siku. NMB ilikabidhi pikipiki 5 aina ya Honda mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini - Ernest Mangu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Chiku Galawa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi – Mathias Chikawe akiwasha pikipiki iliyotolewa na benki ya NMB kwa jeshi la polisi ili kusaidia operation za kila siku huku akishuhudiwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Boghols. NMB ilikabidhi pikipiki 5 aina ya Honda mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini - Ernest Mangu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Chiku Galawa.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Boghols akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Ernest Mangu wakati walipokutana mjini Dodoma kulikokuwa kukifanyika Mkutano Mkuu wa Maafisha waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...