Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) walijumuika kwa pamoja katika uwanja wa jamhuri mjini Dodoma kwa ajili ya kushiriki tamasha maalum kwa ajili ya kuwapongeza watumishi wenzao ambao waliiwakilisha vyema wizara katika mashindano ya SHIMIWI na SHIMISEMITA iliyofanyika mwaka jana.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bwana Mohamed Pawaga. Tamasha hilo liliambatana na kufanyika kwa michezo mbalimbali kama vile Mpira wa Miguu, Netiboli, Kuvuta kamba na Riadha.
Katika mchezo wa mpira wa miguu, timu ya mpira wa miguu kutoka jengo la SOKOINE ilifanikiwa kuilaza timu kutoka jengo la Mkapa kwa mabao mawili kwa bila. Mabao ya washindi yakiwekwa wavuni na Abdallah Mbuguni na Ally Kiama. Kwa upande wa Netiboli, timu ya Jengo la Mkapa iliigalagaza timu ya Sokoine kwa magoli 19 kwa mawili. Katika mchezo wa kuvutana kamba, timu hizo zilitoshana nguvu kwani kila timu ilishinda awamu moja.

Katika mchezo wa riadha wanaume, mkimbiaji Philbert Rwakilomba kutoka jengo la Mkapa alishinda mbio za mita 200, na kufuatiwa na Ebeneza mlinga pia wa jengo la Mkapa na nafasi ya tatu ilishikwa na Felix changwe kutoka jengo la Sokoine. Kwa upande wa wanawake florah Odilo alishika nafasi ya kwanza, na kufuatiwa na Yadesi Katamba na chiploe Mpelembe wote kutoka jengo la Mkapa.
Katika mbio za mita 100 wanaume, nafasi ya kwanza ilishikwa na Christopher masomapya kutoka jengo la Mkapa, huku nafasi ya pili ikienda kwa Donath kambanyuma na nafasi ya tatu Jeremiah Mtawa wote kutoka jengo la Sokoine

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...