Kilio cha watanzania hususani wakazi wa jiji la Dar ni kero ya upatikaji Majisafi na Salama kwa matumizi
mbalimbali. Kumekuwa na sababu nyingi zinazochangia wananchi kutopata Maji hayo ikiwemo sababu ya
uharibifu wa Miundombinu kwa wananchi wasiokuwa waaminifu kwa kukata mabomba na kujiunganishia
Maji kiholela.
Kiwango cha Maji kinachopotea kwa mujibu wa DAWASCO ni kwa asilimia 54 ambapo kiwango hicho ni
kikubwa zaidi kutoka kile cha kimataifa cha asilimia 16 kinachotakiwa.
Ofisa uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro (pichani) akiongea na waandishi mapema wiki hii alibainisha
kuwa shirika limejipanga kwamba ifikapo 2020 kiwango cha Maji kinachopotea kiwe hakitozidi asilimia 25 ili
kuwawezesha wananchi wengine kupata huduma hiyo.
“ipo mikakati mingi na mizuri ya kuhakikisha maji hayapotei ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa viongozi
wa wananchi tukianzia kwenye ngazi ya Madiwani na watendaji wa serikali za mitaa ili waweze
kuwaelimisha wananchi juu ya udhibiti upotevu wa Maji” alisema Lyaro.
Alisema 2015/2016 imeweka mikakati madhubuti na pia imejipanga kuhakikisha wizi wa maji unapungua ili
kurudisha huduma hiyo kwa wananchi ambao wameikosa kutokana na hujuma ya wananchi wachache.
“Hivyo basi kutokana na kwamba tayari tumewabaini watu wanaofanya vitendo hivyo mwaka huu
tumejipanga kuingia mtaani zaidi na kuhakikisha tunazungukia maeneo yote na tunapogundua kuwepo kwa
tatizo hilo tunawachukulia hatua za kisheria” aliongeza Lyaro.
Wito kwa wananchi ni kushirikiana na DAWASCO katika kutoa taarifa za mara kwa mara pindi uhujumu wa
miundo mbinu ya Maji na wizi wa Maji unapofanyika ili kujenga jamii yenye upatikanaji wa huduma hii kwa
usawa na haki kwani maji ni Uhai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...