Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayoshuhulikia utafiti katika ufumbuzi wa matekeo makubwa na ya haraka Bw.Omari Issa kutoka Tanzania Bara wakati alipokuwa akitoa mada yake wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akiwa Mwenyekiti wa Semina hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifungua semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini,ufunguzi huo ulifanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kuwashirikisha Viongzi wa ngazi za juu wa serikali ya Mapinduzi wakiwemo Mawaziri,Naibu Mawaziri,Makatibu Wakuu,Naibu Makatibu Wakuu na Watendaji wengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...