Mkuu wa Hazina wa Benki ya
Exim, George Shumbusho, akikata utepe kutambulisha kadi ya “Faida EMV
Debit Card” itakayochukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua
ikitumika hapo awali. Ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha kudhibiti majanga wa
Benki ya Exim, David Lusala (kulia) na Afisa masoko wa benki hiyo,
Noel Tuga. Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo
wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa
kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti
majanga wa Benki ya Exim, David Lusala (kulia),akisisitiza jambo
wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam
jana, kutambulisha kadi ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua
nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali.
Kushoto ni Mkuu wa Hazina wa benki hiyo, George Shumbusho. Kadi hiyo hutoa
usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua
taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu
unakili wa taarifa za mteja husika.
Mkuu wa Hazina wa Benki ya
Exim, George Shumbusho (kushoto), akisisitiza jambo wakati wa
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana,
kutambulisha kadi ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi
ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Kulia ni Mkuu
wa Kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki hiyo, David Lusala.
Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’
inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo
kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
Katika jitihada za kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki
kwa wateja wake katika mazingira salama zaidia Benki ya Exim imetambulisha kadi
mpya ya kimataifa ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya
“Magnetic Stripe Faida Debit Card” zilizokua zikitumika hapo awali.
Kadi hiyo mpya hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa
‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja ikiwa na mfumo madhubuti wa
kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika. Hii itasaidia
wateja wa benki hiyo kutekeleza miamala yao katika mfumo ulio salama zaidi.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Hazina
wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho alisema kadi hiyo mpya ina usalama
ulioimarishwa zaidi kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ na kufanyika kwa
ukaguzi wa ziada wa namba ya siri.
“Tunatambua hitaji la wateja wetu kuweza kufanya miamala yao kwa
usalama zaidi. Kwa kutumia kadi hii mpya ya kimataifa kutoka Benki ya Exim,
mteja anaweza kuwa na uhakika kwamba miamala yake inafanyika katika mazingira
salama kabisa,” alisema Bw. Shumbusho.
Aliongeza kuwa, Kadi hiyo mpya ya kimataifa inamuwezesha mteja
kufanya miamala duniani kote katika mashine za ATM na POS zilizothibitishwa na
MasterCard.
“Kama Benki ya Exim, tunaamini kuwa ugunduzi ni maisha. Hivyo
basi, tutaendelea kugundua teknolojia mpya zitakazoendana na kasi ya ukuaji wa
utandawazi katika dunia hii ya sasa ili kuweza kukabiliana na changamoto
zilizopo katika usalama wa kimtandao.
“Ni matumaini yetu kuwa wateja wetu watazifurahia zaidi kadi zao
mpya za “Faida EMV Debit card,” alisema.
tunashukuru kwa kujidhatiti na usalama hela za wateja ila gharama yake kwa mwaka ni kubwa sana kwa sisi wateja wakawaida, salio linapunguzwa bila makubaliano.
ReplyDelete