KIKOSI cha timu ya Friends
Rangers, kesho kinajitupa kwenye
Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam kuvaana na timu ya
African Lyon, katika mchezo wa
ligi daraja la kwanza.
Ofisa habari wa Friends
Rangers, Asha Kigundula,
alisema kuwa mchezo huo wa
pili kwa timu hizo ikiwa ni
mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Kigundula alisema kuwa kikosi
chao kipo katika hali kubwa ya
kuhakikisha haitapoteza
mchezo huo.
Alisema kikosi chao chini ya
kocha wao Ally Yusuph 'Tigana'
kina matumaini ya kufanya
vizuri katika mchezo huo.
Kigundula alisema licha ya
kutambua ugumu wa mchezo
huo, lakini wana matumaini ya
kufanya vizuri.
Alisema endapo watafungwa au
kutoka sare timu yao itakuwa
imepoteza mwerekeo wa
kupanda daraja.
"Mchezo huo ni lazima
tushinde; tusiposhinda tutakuwa
tumejiweka pabaya zaidi katika
kupanda ligi kuu msimu
ujao"alisema Kigundula.
Rangers inashika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi daraja la kwanza baada ya kupoteza mechi yake dhidi ya Lipuli, kwa kufungwa bao 1-0, kwenye Uwanja wa Samora Mkoani Iringa.
African Lyon
Friends Ranger
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...