Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa
Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakijumuika na wananchi katika
kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukurani kwa Mashekhe wa Bagamoyo na wananchi kwa kumuandalia hafla ya kumuombea dua katika mkesha wa mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiomba dua pamoja na Mashekhe wa
Bagamoyo na wananchi wakati wa hafla ya kumuombea dua katika mkesha
wa mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa jamii ya
wamasai wanaoishi mkoa wa Pwani. Kiongozi mkuu wa jamii hiyo, Laiboni
Tikwa Moreto (wa pili kushoto), Majaliwa Lihalei na Zuberi Tangono
katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze,
Mkoa wa Pwani.
PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...