Makamu wa Rais wa Isaca Tanzania Chapter ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao, Dk. Jabir Bakari akitoa hotuba yake wakati akifungu semina kuhusu usalama wa mifumo ya kompyuta pamoja na ukaguzi wa mifumo hiyo kwa kuwakutanisha wataalumu na kujadiliana kuhusu ukuaji wa teknolojia na usalama.
Aidha Dk. Jabir alisema kuwa semina hiyo inawakutanisha wataalamu wa mifumo ya kompyuta kutoka ndani na nje ya nchi watakaojifunza na kuongeza utaalamu wa kulinda mifumo ya mitandao.
Naye Mratibu wa Semina hiyo ambaye pia ni Rais wa Isaca Tanzania, alisema kuwa semina hiyo kwa ajili ya kuelezea wadau wa mitandao kuhusu mwelekeo wa teknolojia duniani na ukubwa wa tatizo katika wizi wa mitandao 'miaka ya nyuma kulikuwa na wizi wa kuvunja katika mabenki lakini siku hizi mbinu za wizi zimebadilika na wezi wanaiba kupitia mifumo ua mitandano hasa kompyuta pamoja na simu, kutoa elimu ya ajili ya mifumo ya kompyuta namna ya kuilinda na kuiendeleza.
Katibu wa Tanzania Chapter, Nemayani Kaduma (kulia)akiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina ya ya kimataifa kuhusu usalama wa mitandao wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Taasisi ya Isaca Tanzania Chapter, Dk. Jabiri Bakari (hayupo pichani) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Bongo watu wamenuna nuna tu
ReplyDeleteMaisha magumu sana
ReplyDelete