Ktibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Wanachama wa kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara mara baada ya kushiriki kupanda Migomba,katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.

 katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda Mgomba katika shamba la Kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga  katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.
 Mbunge wa Jimbo la Chaani,Mh.Ally Juma Haji a.k.a Chepe akizungumza na baadhi ya vijana kuhusiana mambo mbalimbali ikiwemo na kuwahimiza kupiga kura ya ndio kwa katiba inayopendekezwa.
 Baadhi ya Wananchi wanaoshiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mapema leo.Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.7 ina thamani ya shilingi milioni 26
 Katibu mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.7 yenye thamani ya shilingi milioni 26
Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini katika jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80 ukiendelea,Mradi huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini,jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80.Mradi huo huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Banda Maji mara baada ya kupokea taarifa ya kikundi cha ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga,pia kushiriki kazi ya kilimo cha Migomba na Mbogamboga,katika Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.

PICHA NA MICHUZI JR-KASKAZINI UNGUJA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...