Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa kwa wananchi na Vyombo vya Habari kuhusu mgogoro wa eneo la TONDORONI lililopo katika Wilaya ya Kisarawe kama ilivyokaririwa na baadhi ya Vyombo vya Habari hapa nchini.

Taarifa zilizotolewa na kukaririwa na baadhi ya Vyombo vya Habari kwamba Wanajeshi wametumia nguvu kuwatoa wananchi eneo la TONDORONI na baadhi yao kudai kupotelewa na mali zao siyo za kweli na ni za kuwapotosha wananchi kwa sababu wananchi hao walitaarifiwa kuondoka kupitia uongozi wa Wilaya na uongozi wa Vijiji vya MLOGANZILA na KILUVYA B. Aidha, walipewa muda wa kutoa vitu vyao na wao kuondoka.

 JWTZ linapenda kuwahakikishia wananchi kuwa hatua ya kuwaondoa wananchi wavamizi kutoka katika eneo la kambi ya Jeshi kwa uangalifu, umakini na kulikuwa na usimamizi wa hali ya juu na hakuna mali ya mwananchi iliyoporwa kama ilivyodaiwa. 

Ifahamike kwamba; Jeshi linaona ni bora lilaumiwe kwa kuwaondoa wananchi waliovamia  maeneo hatarishi  ya jeshi ambayo hutumika katika mafunzo yanayohusisha risasi za moto,  zana hatari za kijeshi  na mabomu ambayo wakati mwingine hulipuka baada ya muda fulani kupita badala ya kuwaacha wakae katika maeneo hayo  kutokana na sababu za kisiasa au ushabiki mwingineo na hivyo kuwa katika hatari ya kuweza kuumia vibaya au kupoteza maisha yao na mali zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...