Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia
na Watoto, Mhe. Sophia Simba (katikati) akimsikiliza Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi.Gracia
Machel (wa kwanza kushoto) aliyefika Wizarani hapo kujadili program maalum ya
kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu.
Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia
na Watoto, Mhe. Sophia Simba (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao chake
na aliyekuwa Rais wa
Afrika ya Kusini Bi.Gracia Machel (wa kwanza kushoto) aliyefika Wizarani hapo
kujadili program maalum ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu. Wengine
kulia ni wa kwanza kulia ni Kulia ni
Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , Nuru
Millao na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto, Benedict Missani.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba ( katikati) na Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini
Bi.Gracia Machel wa kwanza kushoto
wakiongea jambo wakati Mama
Machel alipofika wizarani wakati wa ziara yake nchini. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , Nuru Millao.
==== ===== ======
Mke
wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi. Gracia Machel yuko nchini katika
ziara fupi kusaidia kumaliza tatizo la Ndoa za utotoni kupitia programu na miradi
mbalimbali atakayoifadhili ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu hatimae
kujikomboa na umaskini.
Katika
ziara yake mama Machel, amekutana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Mhe. Sophia Simba ambapo, alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya
Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa jitihada
kubwa inayofanya wizara hiyo kupambana na tatizo hilo la mimba za utotoni.
Vilevile,
aliitaka Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto na wadau
mbalimbali hususan viongozi wa mila/jadi na dini kushirikiana nae na kuwa mstari wa mbele katika
kuleta mabadiliko chanya kupitia program hizo anazotarajia kuzianzisha, na kuongeza kuwa, “Mkoa wa Mara ndio utakaokuwa
wa kwanza kuanzishwa kwa program hiyo kwani bado mkoa huo una mila gandamizi.
(mfumo dume)”,alisema Machel.
Naye
Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akiongea
katika kikao hicho, alieleza kuwa, ni kweli tatizo hilo lipo nchini lakini
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali, Asasi za Kiraia na vyombo vya habari, wanapambana kikamilifu
kumaliza tatizo hilo.
Aidha,
Waziri Simba alitumia fursa hiyo kumshukuru Mama Machel kwa jitihada
anazozifanya kuwawezesha watoto wa kike kuondokana na umaskini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...