Na Faustine Ruta, Mwanza
Timu ya Wanawake kutoka Mkoa wa Kagera imetupwa nje ya Mashindano kwa Matuta baada ya kumaliza mtanange wao kwa sare ya Nyumbani ya Ushindi wa 2-1 na Ugenini,CCM Kirumba Mwanza na Matuta kupigwa na Timu ya Mwanza kuibuka na Ushindi wa bao 4-3.
Mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Timu ya Mwanza ndio walianza kupata bao mapema dakika ya 2 kupitia kwa mchezaji wao matata Meriam Kimbuya (10) kwa kukatiza katikati ya mabeki na kufunga bao hilo la kwanza. Kipindi cha pili mchezaji huyo huyo Meriam Kimbuya aliwafungia bao tena Mwanza katika dakika ya 64 na kufanya 2-0 dhidi ya timu ya Kagera. Kagera waliongeza Bidii na dakika ya 73 Mchezaji Anna Katunzi aliachia shuti kali lililomzidi nguvu kipa wa Mwanza na kuishilia nyavuni na kufanya 2-1.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...