Mkugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Rehan Athumani (katikati) akifungua semina ya siku tatu Januari 21, 2015 jijini Dar es Salaam ya viongozi wa SACCOS za wajasiriamali zilipo Mansipaa ya Ilala iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lengo la semina hiyo kuwapa elimu viongozi hao kuhusu Mfuko Taifa wa Bima ya Afya ili wapeleke ujumbe kwa wanachama wa SACCOS waweze kujiunga na mfuko huo (kushoto) Afisa Ushirika Mansipaa ya Ilala, Ladislaus Mwamanswao (kulia) Meneja wa CHF Bima ya Afya, Costantine Makala.
Afisa Matekelezo wa NHIF, Godfrey Tumaini akiwakilisha mada yake kuhusina mpango wa kikoa ambapo amesema mpango huo ni mpya na umeanzishwa kwa malengo ya kukidhi haja ya kundi la watu wa kati ambao hawawezi kujilipia bima kama watu binafsi na hawaridhiki kujiunga katika mfumo wa CHF katika mfuko huo.
Afisa Matekelezo NHIF Mansipaa ya Ilala, Hipoliti Lello akisisitiza jambo wakati wa semina ya siku tatu Januari 21, 2015 jijini Dar es Salaam ya viongozi wa SACCOS za wajasiriamali zilipo Mansipaa ya Ilala iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lengo la semina hiyo kuwapa elimu viongozi hao kuhusu Mfuko Taifa wa Bima ya Afya ili wapeleke ujumbe kwa wanachama waweze kujiunga na mfuko huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...