Na Mwandishi Wetu

KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania (Trafic), Mohamed Mpinga (pichani), ametoa onyo kwa  baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuthibitika kama zina ukweli ndani yake.

Kamanda Mpinga, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la baadhi ya mitando kusambaza taarifa kuwa kulikuwa na basi la Kampuni ya Dar Express limepata ajali.

Alisema, onyo hilo linatokana na kitendo cha baadhi ya mitandao hiyo, jana kusambaza taarifa kuwa kulitokea ajali iliyohusisha gari namba T 640 AXL, huku ikishindwa kutoa ufafanuzi ilikotokea jambo ambalo limezua taharuki kwa abiria wanaotumia mabasi ya kampuni hiyo.

Mitandao iliyohusika katika kusambaza picha za ajali hiyo ya uzushi ni Bongo Mzuka, Whatsapp, Facebook na Jamii Forum. 

“Baada ya picha ya basi hilo kusambazwa katika mitandao hii nilipigiwa simu na baadhi ya watu wakitaka kujua kama ni kweli kulikuwa na ajali kama hiyo, iliwaweze kujua majaliwa ya ndugu zao walio kuwa safarini wakitumia mabasi ya kampuni hiyo,”alisema Mpinga.

Mpinga, aliwatoa hofu wananchi kuwa hakuna ajali yeyote iliyotokea ambayo ilihusisha basi la kampuni hiyo katika siku za hivi karibuni na kwamba gari lililooneshwa katika mitandao ni la uongo kwa vile haliko barabarani. 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Dar Express,Yudika Mremi
“Niwashauri wamiliki hawa kuwa wajaribu kuwa makini na waitumie mitandao kwa ajili ya manufaa yao na watu wengune lakini si kwa matumizi kama haya ambayo yanaweza kuwaletea wengine madhara katika maisha yao na ieleweke watu wa aina hiyo wakipatikana watafikishwa katika vyombo vya sheria,”alisema.


Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dar Express, Yudika Mremi 
alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi wa ajali hiyo, alisema hata yeye alishtushwa na taarifa hizo, kwa vile gari lililooneshwa katika mitandao hiyo lilipata ajali miaka mitano iliyopita pia haliko tena barabarani tangu kipindi hicho.

Alisema baada ya kuona picha hizo alichofanya alikwenda Kituo cha Polisi Kinondoni, kufungua jalada kwa ajili ya polisi kufanya uchunguzi ambao utasaidia kujua nia ya watu waliotoa taarifa hiyo ya uongo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Yote hii ni kutafuta umaarufu tu bila kuelewa athari na usumbufu kwa jamii nzima. Tuwe na utu jamani

    ReplyDelete
  2. Hamna shida, wacha mitandao ijichuje mpaka hapo tutakapobaki na mitandao inayoheshimika katika jamii kwa umakini wa uhabarishaji!! Hata TV zilipoanza uko majuu, vilitokea vikampuni vingi sana, lakini sasa mchujo umepita na kupatikana vituo vya uhakika!!

    Hapa tatizo ni ile kutaka kuwa wa kwanza!! Tutajua tu nani mkurupukaji, na ni nani mwenye fani ya uhabarishaji. Time will tell!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...