KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania (Trafic),
Mohamed Mpinga (pichani), ametoa onyo kwa baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa
ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuthibitika kama zina ukweli ndani yake.
Kamanda Mpinga, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la baadhi ya
mitando kusambaza taarifa kuwa kulikuwa na basi la Kampuni ya Dar Express limepata
ajali.
Alisema, onyo hilo linatokana na kitendo cha baadhi
ya mitandao hiyo, jana kusambaza taarifa kuwa kulitokea ajali iliyohusisha gari
namba T 640 AXL, huku ikishindwa kutoa ufafanuzi ilikotokea jambo ambalo
limezua taharuki kwa abiria wanaotumia mabasi ya kampuni hiyo.
Mitandao iliyohusika katika kusambaza picha za ajali
hiyo ya uzushi ni Bongo Mzuka, Whatsapp, Facebook na Jamii Forum.
“Baada ya picha ya basi hilo kusambazwa katika
mitandao hii nilipigiwa simu na baadhi ya watu wakitaka kujua kama ni kweli
kulikuwa na ajali kama hiyo, iliwaweze kujua majaliwa ya ndugu zao walio kuwa
safarini wakitumia mabasi ya kampuni hiyo,”alisema Mpinga.
Mpinga, aliwatoa hofu wananchi kuwa hakuna ajali
yeyote iliyotokea ambayo ilihusisha basi la kampuni hiyo katika siku za hivi
karibuni na kwamba gari lililooneshwa katika mitandao ni la uongo kwa vile
haliko barabarani.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dar Express,Yudika Mremi
|
“Niwashauri wamiliki hawa kuwa wajaribu kuwa makini
na waitumie mitandao kwa ajili ya manufaa yao na watu wengune lakini si kwa
matumizi kama haya ambayo yanaweza kuwaletea wengine madhara katika maisha yao
na ieleweke watu wa aina hiyo wakipatikana watafikishwa katika vyombo vya
sheria,”alisema.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dar Express, Yudika Mremi
alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi wa ajali hiyo, alisema hata yeye alishtushwa
na taarifa hizo, kwa vile gari lililooneshwa katika mitandao hiyo lilipata
ajali miaka mitano iliyopita pia haliko tena barabarani tangu kipindi hicho.
Alisema baada ya kuona picha hizo alichofanya
alikwenda Kituo cha Polisi Kinondoni, kufungua jalada kwa ajili ya polisi
kufanya uchunguzi ambao utasaidia kujua nia ya watu waliotoa taarifa hiyo ya
uongo.
Yote hii ni kutafuta umaarufu tu bila kuelewa athari na usumbufu kwa jamii nzima. Tuwe na utu jamani
ReplyDeleteHamna shida, wacha mitandao ijichuje mpaka hapo tutakapobaki na mitandao inayoheshimika katika jamii kwa umakini wa uhabarishaji!! Hata TV zilipoanza uko majuu, vilitokea vikampuni vingi sana, lakini sasa mchujo umepita na kupatikana vituo vya uhakika!!
ReplyDeleteHapa tatizo ni ile kutaka kuwa wa kwanza!! Tutajua tu nani mkurupukaji, na ni nani mwenye fani ya uhabarishaji. Time will tell!