Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu (kushoto) akimuongoza Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi aliyeambatana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kuwasili ofisi za Mradi wa Maji Kibiti ulioko wilayani humo mkoani Pwani kabla ya kuukagua.Ukaguzi wa mradi huo ni sehemu ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara inayofanywa na wajumbe wa Kamati hiyo.
Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati Amina Makilagi akipanda ngazi za tanki la maji la mradi wa maji wa Kibiti wakati akikagua mradi huo, huku Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu na watendaji wengine wakishuhudia.
Huyu mama jasiri kupanda ngazi na kitenge.
ReplyDeleteMdau wa mwanzo hapo juu usinifurahishe, tena mguuni na ka 'skuna' kake bila woga. Pengine hakutarajia kama kuna kuparamia huko juu ya hilo 'tangi' huenda angekuja kavalia' accordingly'. Hata hivyo hongera sana mwanakamati Bi Amina Makilagi kupanda na kuteremka salama.
ReplyDeleteUongozi taabu imemlazibu kupanda
ReplyDelete