Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia sehemu ya wakazi wa Nungwi na Wafuasi wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Skuli,jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.Kinana amewataka Wananchi hao kuwa makini na baadhi ya viongozi wenye tamaa ya madaraka kwa kuahidiwa mambo ambayo hayatekelezeki,pia amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi siku ikifika ya kupiga kura ya ndiyo kwa katiba inayopendekezwa,kwani imejaa mambo mengi na mazuri kwa Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Nungwi na Wafuasi wa CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipowahutubia mapema leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Skuli,jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Skuli,Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.Nae amewataka vijana kuacha tabia yakushabikia vyama ambavyo havina msaada kwao
Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Nungwi akiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,aliwahutubia mapema leo jioni kwenye uwanja wa Skuli,jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.
Baadhi ya Wanachama wapya wapatao 284 waliojiunga na chama CCM wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama
Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...