Familia ya Luteni Kanali Willy John Masoi (Mstaafu) wa
Sabasaba Ukonga, Dar es Salaam tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu,
jamaa, marafiki na majirani kwa msaada wa hali na mali wakati wa msiba wa Baba
yetu mpendwa Luteni Kanali Willy John Masoi (Mstaafu) aliyefariki dunia Disemba
22, 2014 na kuzikwa Disemba 27, 2014 nyumbani kwake Dar es Salaam.
Aidha shukrani za pekee tunatoa kwa Paroko, uongozi na walei
wa Parokia ya Mt. Augustino ya Ukonga, Uongozi na wanajumuia wa Jumuia ya Mt.
Monica ya Sabasaba Ukonga, Makamanda na Wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), Uongozi na watumishi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
(MAFC), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA),
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (NAOT), Chuo
Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Ofisi ya Umoja wa Mataifa New York.
Tunatoa shukrani za pekee pia kwa Dk. Kaushik Ramaiya, madaktari na wauguzi wa
Hospitali ya Shree Hindu Mandal kwa huduma ya matibabu wakati wa uhai wa Baba
yetu Mpendwa.
Tunatambua pia michango ya kipekee ya wanaukoo wa Masoi na
Minja, familia za Mshanga, Kajiru, Milanzi, Msolla, Msinjili, Leshabari, Mlay
na majirani zao.
“Raha ya milele umpe ee Bwana, na Mwanga wa milele
umwangazie. Apumzike kwa amani”
Amina
“Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo
nimeumaliza, imani
nimeilinda”
(2Tim 4:7)


.jpg)
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa amani. Amina.......Kristu........
ReplyDelete