Katibu
Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana pamoja na wanachama wa CCM wakiwemo na
Wananchi kwa pamoja wakishiriki katika shughuli ya za uchimbaji na
utandazaji wa mabomba ya mradi wa maji safi na salama katika shehia ya
Kilimani,kwenye jimbo la Mjimkongwe.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi ndani ya chumba cha
kufundishia Kompyuta katika kituo cha Vijana (Tanzania Youth Icon),cha
kuwaendeleza na kuwawezesha katika masuala mbalimbali ikiwemo
elimu,Ajira na Michezo kilichopo Shehia ya Miembeni,Mwembemadema katika jimbo la Kikwajuni.
Mwenyekiti
wa Kituo cha Tanzania Youth Icon (TAYI),Bwan.Abdullah Miraji Othman
akisoma hotuba Mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuhusiana na
mambo mbalimbali yahusuyo kituo hicho cha huduma rafiki kwa Vijana
kilichopo Muembemadema ndani ya jimbo la Kikwajuni sambamba na
changamoto wazipatazo juu ya kituo hicho.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza mbele ya wanachama wa chama hicho
pamoja na Wananchi nje ya Kituo cha Tanzania Youth Icon (TAYI),ambapo
mlezi na mhamasishaji wake ni Mbunge wa jimbo la Kikwajuni,Mh.Hamad
Yusuf Masauni.Kituo hicho cha TAYI ni Taasisi ya vyama visivyokuwa vya
kiserikali,ambayo ina muelekeo wa kuwasaidiana na Wadau mbalimbali
katika kufanikisha shughuli za maendeleo.Mwenyekiti wa Kituo cha
Tanzania Youth Icon (TAYI),Bwan.Abdullah Miraji Othman amesema kuwa
Taasisi hiyo hivi sasa ina ina wanachama wasiopungua 500 ambao tayari
wameandikishwa na kuwepo katika rekodi na kumbukumbu za ofisi,Bwana
Abdullah aliongeza kuwa kituo hicho kinawajenga vijana kiuchumi na pia
kuwapa taaluma ya uongozi ili waje kuwa viongozi wazuri ,''kituo hiki
kimekuwa kiwanda kizuri cha kuzalisha vijana wazuri kwa Taifa'',alisema Bwan.Abdullah .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Balozi Ali Karume alipowasili katika Shehia ya Miembeni,katika jimbo la Kikwajuni,ambapo Ndugu Kinana alipokea taarifa fupi ya mradi wa Zahanati na kushiriki katika ujenzi wa Taifa wa Ukarabati wa Zahanati ya Miembeni (Nyumba ya Yasu).Pichani kulia ni Muwakilishi wa jimbo la Kikwajuni,Mh.Mahamoud Mohamed Mussa pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Kikwajuni Mh.HamadiYussuf Massauni
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifurahia jambo na Balozi Ali Karume walipokutana leo katika Shehia ya Miembeni,katika jimbo la Kikwajuni.
Mmoja
wa Mabalozi akifurahi mara baada ya kukabidhiwa baiskeli yake na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa
shughuli mbalimbali za kichama,baiskeli hizo ilikuwa ni ni moja ya
ahadi alizoahidi kutoa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mh Masauni,ambapo
pia alitoa piki piki kwa makatibu wa chama. PICHA NA MICHUZI JR-ZANZIBAR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...