Mratibu wa Mpango wa Kampuni ya Konyagi wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao la zabibu kwa masomo ya Sekondari Saimon Chibehe (katikati), akitembelea hivi karibuni shamba la zabibu la Festo Kuziganika katika Kijiji cha Mbabara, mkoani Dodoma. Kulia ni mmoja wa wakulima wa eneo hilo, Juliana Masukwi. Watoto wa wakulima hao wameingizwa kwenye mpango huo.
 Festo Kuziganika mkazi na mkulima wa zabibu katika katika Kijiji cha Mbabara, Manispaa ya Dodoma akimuelekeza jambo Mratibu wa Mpango wa Kampuni ya Konyagi wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao hilo kwa masomo ya Sekondari,Saimon Chibehe (kulia) aliyekwenda hivi karibuni kuwatembelea wakulima hao.
 Mratibu wa Mpango wa Kampuni ya Konyagi wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao la zabibu kwa masomo ya Sekondari Saimon Chibehe (wa pili kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkulima Juliana Masukwi (kulia), kuhusu utunzaji wa zao hilo, alipotembelea hivi karibuni shamba hilo katika Kijiji cha Mbabara, mkoani Dodoma. Wa pili kushoto ni mmoja wa wakulima wa zabibu katika Kijiji hicho, Festo Kuziganika. Watoto wa wakulima hao wameingizwa kwenye mpango huo wa kulipiwa masomo.
 Mratibu wa Mpango wa Kampuni ya Konyagi wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao la zabibu kwa masomo ya Sekondari Saimon Chibehe (katikati), akitembelea hivi karibuni shamba la zabibu la Festo Kuziganika katika Kijiji cha Mbabara, mkoani Dodoma. Kulia ni mmoja wa wakulima wa eneo hilo, Juliana Masukwi. Watoto wa wakulima hao wameingizwa kwenye mpango huo.
Mkulima Juliana Masukwi mkazi wa Mbabara A', mkoani Dodoma akimuonesha  mti wa mzabibu Mratibu wa Mpango wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao hilo kwa masomo ya SekondariSaimon Chibehe (hayupo pichani), ambaye hivi karibuni alitembelea shamba lake lililomwezesha mtoto wake aanze kufadhiliwa na kampuni ya Konyagi kielimu kwa masomo ya sekondari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nikilinganisha mashamba haya na yale ya mizabibu yaliyoko Australia na Ufaransa inabidi wakulima wetu wapewe mafunzo ili kuongeza uzalishaji wa zabibu kwa kila ekari.


    Maana naona mistari ya mizabibu iliyopandwa kuna sehemu yenye uwazi mkubwa baina ya mche na mche sijui miche mingine ya zabibu ilikufa au vipi?! Hii inapelekea uzalishaji wa chini kwa ekari moja moja.

    Mdau
    Diaspora
    Mjini Le Havre , Ufaransa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...