CASSIAN KIGESO MALIMA
Ni
kama jana tu lakini tayari leo imetimia miaka 6 tangu Mpendwa wetu Cassian
Kigeso Malima ulipotutoka ghafla jioni ya tarehe 9 Januari 2009 katika
hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam
na kupumzishwa katika makao ya milele kwenye makaburi ya Mwisenge, Musoma mjini
tarehe 14 Januari 2009.
Daima
tutakukumbuka kwa upole, ucheshi na uchapakazi wakati wa uhai wako. Tunamuomba
Mungu wa Rehema aendelee kukupumzisha kwake katika amani ya milele. Amina.
1 Wathesalonike 4:13-14 (Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa
akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja
naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai,
tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao
waliokwisha kulala mauti).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...