Na Bashir Yakub
Wiki iliyopita niliandika kuhusu Asilimia kumi ambayo serikali za mitaa huwa wanaidai hasa maeneo ya mijini baada ya wahusika kuwa wameuziana nyumba au kiwanja. Nikasema wazi kabisa bila kungata meno kuwa hiyo pesa iitwayo asilimia kumi au pesa nyingine yoyote mtu atakayolipa serikali za mitaa eti kwakuwa amenunua au ameuza eneo lake ni rushwa.
Na leo nakumbusha na kusisitiza tena kuwa Watanzana wajue ukitoa pesa ile umetoa rushwa na huyo kiongozi wa serikali za mitaa uliyempa amepokea rushwa kwakuwa malipo hayo hayatambuliwi na hayaainishwi na sheria yoyote.
Lazima ifike hatua haya mambo yaeleweke. Pia nimetahadharisha mara nyingi kuhusu umakini unaponunua kiwanja/nyumba na kueleza baadhi ya mambo ambayo ukiyafanya utakuwa umefanya manunuzi salama na utakuwa umeepuka migogoro na hata mgogoro ukitokea wewe hautapoteza. Anayetaka kusoma haya yaliyopita aandike neno MAKALA SHERIA kwenye google ataona makala hizo.
Leo tena naeleza uhalali kisheria wa serikali za mitaa kusimamia mikataba. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
heee!! sasa nani anayetakiwa kusimamia?
ReplyDeleteSababu mimi nilisimamiwa na Mjumbe na Mwenyekiti !!
Na nikapewa kitambulisho cha mkazi Serikali ya mtaa..
Hapo sasa mtanaka ugomvi na oungozi wa serikali za mitaa. Patashika zote katika uchaguzi wa hivi majuzi wengi wamelenga kupata chajuu wakati wa mauziano ya viwanja, mashamba na nyumba!!!
ReplyDeletenyie wataaalamu wa sharia bana, msije mkatuuza, maana serikali inaanzia mtaani, ungesema hivi, tuende serikali za mtaa na tuwe na wanasheria pia, unaweza kuuziwa mbuzi kwenye gunia, juzi jirani yangu kauziwa kiwanja ambacho tayari kimeshauzwa ila mnunuzi wa kwanza alikuwa hajamaliza hela, wakaja wateja kikauzwa tena, sasa hapo ni balaaa. je kama wangemshirikisha mwenyekiti wa mtaa au mjumbe, hiyo kero yote ingetokea wapi?. mie binafsi nadhani ni vizuri kuwashirikisha wote. maana wanaojua mipaka ya wananchi ni wajumbe na wenyeviti. mwanasheria ni mihuri tu. ukigonga muhuri kwenye kiwanja ambacho ni cha mtu je hapo vipi? matapeli siku hizi wengi ndugu yangu. nisaidie kwa hili.
ReplyDeleteNi vizuri kujua kweli huu, endelea kutuelimisha.
ReplyDeleteAsante sana Michuzi kwa kuweka hii makala muhimu ya kuelimisha umma kuhusu sheria ya kuuziana ardhi. Ufumbuzi wa tatizo la rushwa nchini ni elimu kwa wananchi. Hatua kama hii ya kuelimisha wananchi ina uzito mkubwa kwa maendeleo ya taifa letu. Shukrani nyingi kwa Bw. Bashir Yakub mwanasheria anayetayarisha hii makala.
ReplyDelete