Na Bashir Yakub
Wiki  iliyopita  niliandika  kuhusu  Asilimia kumi ambayo  serikali  za mitaa huwa  wanaidai  hasa  maeneo  ya  mijini baada  ya  wahusika  kuwa wameuziana nyumba au  kiwanja. Nikasema  wazi  kabisa  bila  kungata  meno  kuwa  hiyo  pesa iitwayo asilimia kumi au pesa nyingine yoyote   mtu  atakayolipa  serikali  za  mitaa eti  kwakuwa amenunua  au  ameuza   eneo  lake   ni rushwa. 
Na  leo  nakumbusha na  kusisitiza  tena   kuwa  Watanzana wajue   ukitoa   pesa  ile   umetoa  rushwa  na huyo  kiongozi  wa  serikali   za   mitaa uliyempa amepokea rushwa  kwakuwa  malipo  hayo  hayatambuliwi  na hayaainishwi  na sheria  yoyote. 
Lazima ifike   hatua  haya  mambo yaeleweke.   Pia  nimetahadharisha mara nyingi kuhusu  umakini unaponunua  kiwanja/nyumba  na kueleza baadhi ya mambo  ambayo  ukiyafanya utakuwa umefanya manunuzi salama na utakuwa umeepuka migogoro na hata mgogoro ukitokea wewe hautapoteza. Anayetaka kusoma  haya  yaliyopita aandike neno  MAKALA  SHERIA  kwenye google ataona makala  hizo. 
Leo tena  naeleza uhalali kisheria wa serikali za mitaa kusimamia mikataba. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. heee!! sasa nani anayetakiwa kusimamia?

    Sababu mimi nilisimamiwa na Mjumbe na Mwenyekiti !!

    Na nikapewa kitambulisho cha mkazi Serikali ya mtaa..

    ReplyDelete
  2. Hapo sasa mtanaka ugomvi na oungozi wa serikali za mitaa. Patashika zote katika uchaguzi wa hivi majuzi wengi wamelenga kupata chajuu wakati wa mauziano ya viwanja, mashamba na nyumba!!!

    ReplyDelete
  3. nyie wataaalamu wa sharia bana, msije mkatuuza, maana serikali inaanzia mtaani, ungesema hivi, tuende serikali za mtaa na tuwe na wanasheria pia, unaweza kuuziwa mbuzi kwenye gunia, juzi jirani yangu kauziwa kiwanja ambacho tayari kimeshauzwa ila mnunuzi wa kwanza alikuwa hajamaliza hela, wakaja wateja kikauzwa tena, sasa hapo ni balaaa. je kama wangemshirikisha mwenyekiti wa mtaa au mjumbe, hiyo kero yote ingetokea wapi?. mie binafsi nadhani ni vizuri kuwashirikisha wote. maana wanaojua mipaka ya wananchi ni wajumbe na wenyeviti. mwanasheria ni mihuri tu. ukigonga muhuri kwenye kiwanja ambacho ni cha mtu je hapo vipi? matapeli siku hizi wengi ndugu yangu. nisaidie kwa hili.

    ReplyDelete
  4. Ni vizuri kujua kweli huu, endelea kutuelimisha.

    ReplyDelete
  5. Asante sana Michuzi kwa kuweka hii makala muhimu ya kuelimisha umma kuhusu sheria ya kuuziana ardhi. Ufumbuzi wa tatizo la rushwa nchini ni elimu kwa wananchi. Hatua kama hii ya kuelimisha wananchi ina uzito mkubwa kwa maendeleo ya taifa letu. Shukrani nyingi kwa Bw. Bashir Yakub mwanasheria anayetayarisha hii makala.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...