Na Bashir Yakub
Wakati mwingine migogoro ya ardhi inasababishwa na kutojua. Wengi hawajui taratatibu na ndio maana hujikuta wanainga katika matatizo. Moja ya maeneo ambako watu wamekuwa wakipatia matatizo ni huu wakati wa kununua.  
Yapo mambo mengi unapoununua ardhi, nyumba au kiwanja ambayo wewe kama mnunuzi unatakiwa kuyajua na kuyazingatia ili usiingie katika matatizo.  Nimefanya utafiti katika  kesi za  ardhi mahakamani na kugundua kuwa  moja ya eneo baya linalowaingiza watu mkenge ni hili la  mume kuuza nyumba au kiwanja  bila kupata ridhaa ya  mke wake.
Ikumbukwe kuwa  suala la ridhaa hapa sio suala la hiyari isipokuwa ni suala la lazima na la kisheria ambalo kutolitekeleza kwake kunaweza kupelekea mnunuzi kupoteza kile alichokinunua. Ni hatari ndugu na umakini unahitajika.Mume anapouza nyumba/kiwanja kuna kitu huitwa ridhaa ya mwanandoa ambacho ni lazima akisaini, tutaona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mke au Mume wa mnunuzi...kwani lazima iwe ni mume tu anauza???

    ReplyDelete
  2. asante sana kwa darasa zuri na moyo wa kuitumia elimu yako kwa jamii, msisitizo wangu tu hapa ni kwamba hiyo mali lazima iwe ni matrimonial property kwani kuna mali nyingine ambazo si za wanandoa

    ReplyDelete
  3. Ankal, naomba kuuliza mbona hujatuwekea picha na hotuba ya Mh Rais ya Ijumaa iliopita katika sherehe za sherry party na wabalozi?

    ReplyDelete
  4. Unamaanisha mke wa muuzaji

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...