Mshambuliaji Hamis Tambwe amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuchukua hatua stahiki dhidi ya wachezaji wa Ruvu Shooting kwa kitendo cha kumshambulia na kumtolea lugha chafu uwanjani ikiwemo kumbagua kwa kumuita mkimbizi.
Akizungumza Makao Makuu ya klabu ya Yanga iliyopo mtaa wa Twiga na Jangwani leo, Tambwe alisema kuwa kitendo alichofanyiwa ni cha kinyama na anakilaani kwa nguvu zote, na anataka aelezwe wazi iwapo wachezaji kutoka mataifa mengine hawatakiwi kucheza Tanzania.
"Uwanja wa Taifa kuna kamera, matendo mengi sana mabaya tumekuwa tukifanyiwa wachezaji wa kigeni, naamini baada ya mchezo TFF wanakaa kupitia mikanda ya mchezo wanaona kila kitu lakini hakuna adhabu zinazochukuliwa tunavyodhalilishwa na kubaguliwa.
"Nimetukanwa, nimeitwa Mkimbizi, nipo nchini kihalali na nafanya kazi kwa kufuata sheria zote kwa nini waniite mkimbizi, nipo tayari kusema matusi waliyonitukana kwa mabosi wangu na kwa TFF ili hatua stahiki zichukuliwe, mpira sio vita, mpira ni burudani, mpira ni 'fair play', lakini hapa imekuwa ni tofauti.
"Kitendo walichonifanyia ni sawa na kunishikia bastola, ni unyama wa hali ya juu walitaka kuniua, yani wamenikaba nilikuwa naona roho yataka toka, hatukuwa vitani walitakiwa wacheze mpira wa 'profesional' hivi tutaogopa kucheza Tanzania."alisema kwa masikitiko.
"Hawakuja kucheza soka, walikuja kupigana, walinipiga kiwiko, wakanipiga ngumi na mwisho walinikaba shingoni nikaona pumzi zinataka niishia.
Hii ni hatari, kuna mtu anaweza kuanguka akapoteza maisha siku moja. Wale wanajeshi hawaingii uwanjani kucheza soka, wanakwenda kucheza na mwili wa wachezaji wenzao.
That is not fear, wachukuliwe hatua wote walimnyanyasa huyu mchezaji wa kigeni. Haitakiwi watatnzania tuwe wabaguzi. Mbona hata sisi tupo nchi za watu tunaishi lakini hawatunyanyasi kwa matusi na kutukaba koo. Huu ni uonevu kama umeshindwa katika mchezo ni umeshindwa tu kubali kushindwa sio kukaba koo kwa kisingizio cha mkimbizi. Hayo ni matusi kabisa
ReplyDeleteThat is not fear???anonymous wa kwanza nini tena lugha gongana?
ReplyDeleteSi bure soka Tanzania kiwango kinazidi kuboromoka.
ReplyDeleteSoka la kibabe limepitwa na wakati, zama hizi ni kutumia mwili vizuri kumiliki mpira na kutafuta mbinu za kumtoka mchezaji-pinzani au kumzuia mchezaji pinzani-kwa -akili na kutumia mwili siyo ngumi, viwiko au kabala.
Naunga mkono maelezo ya Amisi Tambwe wachezaji, makocha, waamuzi na TFF wasisitize fair-play la mchezo wa soka wa kisasa.
Asante sana kwa usahihi wa lugha Anonymous wa pili. Just a mistake, fair not fear. Thanks very much
ReplyDelete