Imebainika kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni almaarufu viumbe wa ajabu Anunnaki Alien,inayoongoza na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja, imejikuta ipo katika hali ya kukosa usingizi tena baada ya kutakiwa kutumbuiza maomyesho zaidi katika msimu ujao wa joto.
Watayarishaji wa maonyesho makubwa ya nje barani ulaya wanashinikizwa na washabiki wao kuwa ni lazima waipandishe jukwaani Ngoma Africa Band kutokana na mdundo wao wa Bongo dansi.
Mapromota hao baada kuwekwa roho juu na washabiki wao nao wamedhamilia kuwapambanisha washabiki hao na bendi maarufu ya Ngoma Africa band yenye makao yake nchini ujerumani,habari za uhakika zimetonya kuwa bendi hiyo imekubali kuenda kutumbuiza katika nchi za Latvia na Austria na maonyesho mengine katika msimu wa joto.
Hali hiyo ya washabiki kushinikiza katika maonyesho inaifanya bendi ya Ngoma Africa band kuwa katika mzunguko wa maonyesho makubwa na wanamuziki kukosa muda wa kupumzika.
Lakini inasemekana kamanda Ras Makunja na kikosi chake wanauwezo wa aina yake wa kuwamudu washabiki wao waliodata akili na jinamizi la muziki wa dansi wa bongo kule barani ulaya.ffu-ughaibuni pia wanasikika online at www.ngoma-africa.com
naona kamanda aliye ipindia akili kazi yake na vijana wake ffu,kamatieni hapo hapo ffu
ReplyDeleteFFU NA MWENDO WA KASI UGHAIBUNI,WASHABIKI WENU WANATISHIA MAISHA MAPOROMOTA
ReplyDeleteNgoma Africa band nakumbushia sisi washabiki wenu wa diaspora Amerika ya Kaskazini na Kusini juu ya kufanya kweli mfungue account maalum ya Ngoma Africa Band YouTube ili nasi tulio mbali na Ulaya na Afrika tusikose uhondo wa Bongo Dansi.
ReplyDeleteTayari mshasema mpo tayari kwa kukabilia kwa vitendo, shindikizo toka kwa mashabiki /wadau wenu hivyo ni imani mtafanya kweli Youtube.
Mdau
Diaspora Amerika ya Kaskazini