Waziri mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa mkono wa pole kwa waombolezaji katika Msiba wa aliekuwa muasisi na kiongozi wa kwanza wa Chama Cha TAA na baadaye TANU wilayani Monduli,Marehemu Mzee Lazaro Ole Ngoilenya Laizer aliyefariki juzi na kuzikwa leo Alhamis kijijini kwake Ngarash Monduli.Marehemu Mzee Lazaro Ole Ngoilenya Laizer ambaye ndiye alikuwa chachu kwa Mh. Lowassa na wanasiasa wengine wa Monduli kuingia katika siasa,amefariki akiwa na umri wa miaka 120,alioa wake 9 na kufanikiwa kupata watoto 53.
Waziri mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa mkono wa pole kwa wajane wa Marehemu.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mzee Lazaro ole Ngoilenya Laizer aliyefariki juzi na kuzikwa leo Alhamis kijijini kwake Ngarash Monduli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...