Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi jijini Mbeya na kufanikiwa kutembelea vyanzo mvali mbali vya maji vilivyo chini ya Mamlaka ya Maji Safi jijini humo.
Mh. Makalla amevutiwa sana na utendaji kazi wa Mamlaka hiyo na kuupongeza kwa kuongeza idadi kuwa wateja wa maji kutoka 9000 mwaka 2002 na kufikia 40,000 hivi sasa na pia kuwa mamlaka ya tatu kitaifa kuwa na miundombinu ya majitaka.
Mh. Makalla ameiagiza Mamlaka hiyo kuhakikisha inadhibiti upotevu wa maji kutoka asilimia 34 ya sasa na wafikie kiwango cha kimataifa asilimia 20.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla (katikati) akimsikiliza Ing. Martin Kimambo wakati akimwonyesha na kumpa maelezo kuhusu miundombinu ya maji taka eneo la Kalobe.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akiangalia chujio la maji eneo la Swaya.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...