Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP Valentino Mlowola akiwa na makamanda wenzake SACP Charles Mkumbo (Shinyanga) na SACP Justus Kamugisha (Simiyu) wakati wakizungumza na waandishi wa habari kufuatia kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa wa ujambazi ambaye pia ni mfanyabiashara aitwaye Njile Samweli (46) marufu kwa “John” wa mjini Bariadi mkoani Simiyu, aliyekuwa akifanya matukio ya uhalifu katika Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida na Tabora.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,SACP Charles Mkumbo akionesha silaha iliyokuwa ikitumiwa katika harakati za matukio ya ujambazi katika kijiji cha Idukilo Kata ya Luhumbo Mwadui wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga.Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP Valentino Mlowola na kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,SACP Justus Kamugisha.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SCP Charles Mkumbo akionesha nguo ambazo zilikutwa kwa Mtuhumiwa kiongozi huyo wa genge la uhalifu ambazo zinasemekana ni za baadhi ya watu waliouawa wakiwemo majambazi aliokuwa akishirikiana nao ambao aliwauwa kwa maslahi yake.
Sehemu ya vitu vilivyokutwa kwa mtuhumiwa huyo.
Hivi Tanzania hii ufanye tukio alafu wasikujue kweli miaka yote?! Anyway huyo wanamjua siku nyiingi tu sema wamemchoka na ndio maana amekamatwa bwana...Majambazi yoote yanajulikana wapi yalipo, mfano yale Majambazi ya katikati kama unaenda Bukoba yapo wapi siku hizi?! si baada ya hao Polisi wakubwa kukemewa na namba moja ndio wakatokomezwa ila kabla ya hapo si siku zote si walikuwepo na kulindwa!
ReplyDeletePolisi mmefanya kazi nzuri kumkamata mshukiwa wa ujambazi lakini mashaka yangu ni kuwa,je hamkuharibu ushahidi(alama za vidole)?.Hii ni kwa sababu wakati wa ukamataji ninaamini hamkuwa na latent gloves kama alivyovaa Kamanda.Kama mlikuwa mmevaa basi kesi hii itafanikiwa kwa mtuhumiwa kutiwa hatiani.Lakini pia publicity haisaidii kupunguza uharifu nchini.Ushauri ni kwamba kazi ifanyike kwa weledi na kutumia bora na kisasa za kiuchunguzi ili kukabiliana na matukio haya.
ReplyDelete