
Kikosi cha Timu ya Mara (jezi Nyekundu) wakisalimiana na Marefa wa mchezo huo tayari kwa Mtanange wa Women Taifa Cup kuzinduliwa leo jijini Mwanza kwa Kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Mh Jamal Malinzi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Mara kabla ya Mechi ya Uzinduzi wa mashindano ya Mpira wa Miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Women Taifa Cup kuanza katika dimba la CCM kirumba leo Jijini Mwanza

Baadhi ya Viongozi wa Mpira wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Viongozi wa TFF na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo Wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Mechi ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Women Taifa Cup kuanza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.

Kikosi Cha Timu ya Mwanza kikiwa tayari kukabiliana na Timu ya Musoma

Hivi pozi la wimbo wa taifa ni lipi naona viongozi kila mtu na lwake! mwingine mikono mbele, wengine vifuani, wengine mikono HIMA!.....
ReplyDelete