Mrakibu msaidizi wa Jeshi la polisi (ACP) mkuu wa kitengo cha elimu kwa umma makao makuu ya usalama barabarani jijini Dar-es-salaam,Abel Swai,akiwahamasisha abiria wa basi la kampuni ya France line lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Arusha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi endapo watagundua dereva mlevi au akiendesha gari vibaya,ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya"Wait to send"inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
PC.Abdalah Ramadhani kutoka trafiki makao makuu Dar-es-salaam,akitumia chombo maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati zoezi la kampeni ya"Wait to send" lililofanyika katika kituo cha mabasi cha Misuna Singida mjini inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Zoezi zuri la kudhibiti uendeshaji wa magari wakati dereva kalewa.Ila naomba kuuliza hivyo vidude vya kupuliza naona vinatiwa mdomoni! je ni disposable au tunasafisha baada ya kutumia.Nilikuwa naaribu kujiuliza kwa sauti tu katika kujali afya za watumiaji!!Naomba kueleweshwa.
ReplyDeleteHivi vimashine vya kumpima pombe nauliza watu siwanaweza kuambukizana TB labda kama hicho kibomba cha plastic kinabadilishwa kwa kila mtu mpya anayepimwa
ReplyDelete