Naibu waziri Maji Mhe Amos Makalla leo amefanya ziara ya kustukiza mkoa Dar es salaam, ambapo amekamata wezi wa maji 12, amewatimua kazi mameneja wa maji Boko na Kimara na pia ametangaza operasheni kubwa zaidi ya kusaka wezi wa maji jijini Dar es salaam
 Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akiangalia miundombinu ya wizi wa maji Magomeni
 Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akitembelea kitongoji cha Manzese kusaka wezi wa maji
 Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla  akiangalia matenki yanayoingizwa maji ya wizi manzese
 Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla  akimsikiliza Mwananchi akielezea jinsi wizi wa maji unavyoendelea Manzese
Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla  akiwa katika operesheni ya kusaka wezi wa maji Boko

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hili ni jambo la kushangaza sana. Kama waziri anatoka wizarani na akafanikiwa kukamata hao wezi huyo Director Bw Midala anafanya nini? Na kwanini awaondoe hao mameneja amwache yeye (Midala)? Tuwe na tabia ya kuwajibika WaTanzania. Hii ina maana ya kuwa Mh Makala akichukua hiyo ofisi ya Dawasco kwa takribani miezi sita na akawa na hiyo tabia ya kuingia mitaani tatizo la wizi wa maji lingepungua kama sio kuisha. Mh Makala nakusaluti kwa hilo na chukua hatua mpaka kwa vigogo wanaopanga sera na huyo Mkurugenzi wao. Kazi nzuri na endeleza zaidi.

    ReplyDelete
  2. Completely waste of resources. Hapa ndipo siasa zinapoingia kwenye mambo yanayohitaji umakini. Ni waziri asiyemakini pekee anayefanya mambo kama haya. Kwa kifupi WALIO CHINI YAKO MHESHIMIWA WAZIRI HAWAFANYI KAZI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...