Picha ya pamoja ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika baada ya Mkutano wao kufunguliwa rasmi jijini Addis Ababa leo.

Na Ally Kondo, Addis Ababa
Kamati ya Uongozi ya NEPAD imekutana leo Jumatatu jijini Addis Ababa, Ethiopia kutathmini utekelezaji wa programu mbalimbali wa chombo hicho. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shuguli za NEPAD kwa mwaka 2014, Mtendaji Mkuu wa NEPAD, Dkt. Ibrahim Mayaki alieleza kuwa Chombo hicho kimepiga hatua kubwa katika maeneo ya kipaumbele iliyojiwekea.

Kwa upande wa miundombinu, Dkt. Mayaki alikumbusha Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliofanyika Darker, Senegal ambao ulijadili njia za kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya miuondombinu barani Afrika. Mkutano huo uliweka msingi wa kuainisha miradi 16 ya miundombinu yenye kukopesheka na yenye lengo la kupunguza tatizo la miundombinu barani Afrika. NEPAD kwa kuzingatia ushauri wa Wakuu wa Nchi, imeanzisha chombo maalum ambacho jukumu lake ni kutoa msaada wa kiufundi katika hatua za mwanzo za maandalizi ya miradi ya miundombinu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...