Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

Waziri wa Nishati na Madini ,George Simbachawene amesema kuwa watanzania wamuamini ataendeleza kwa kasi ile ile katika kuwafikishia wananchi maendeleo kupitia sekta za nishati na madini.

Hayo ameyasema leo wakati alipoanza kazi rasmi katika Wizara hiyo akichukua nafasi ya Profesa Sospeter Muhogo aliyejiuzulu wiki iliyopita,amesema kila mtu sio mkamilifu hata mitume watu wengine hawakumuamini.

Simbachawene amesema ana uzoefu wa kufanya kazi na kuachana na vyeti kwani vyeti ni ziada lakini kalama ya uongozi ndiyo inayohitajika.

Aidha amesema wanaotilia shaka uteuzi wake watakuwa na kigezo lakini kila mtu hawezi kuamini kila binadamu ana mapungufu kwa namna anavyoona mtu.

Simbachawene amesema atafuatilia usiri wa mikataba lakini sasa anasoma mazingira kwanza na kuweza kuweka bayana suala hilo.

“Niko hapa watu waniamini kutokana na kazi zangu na watanzania waniamini niweze kufanya kazi niliyoaminiwa kwa niaba ya watanzania wenzangu”amesema Simbachawene.
Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokelewa na uongozi wa Wizara hiyo mapema leo asubuhi. Mhe. Simbachawene amesisitiza umuhimu wa sekta za nishati na madini kama mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta za nishati na madini.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari mada baada ya kuwasili Wizarani hapo mapema leo asubuhi.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Endeleza kazi nzuri ya kupanua uwekezaji ili watanzania wengi zaidi wapate umeme wa kuaminika mijini na vijijini. Wafanyabishara mipango yao isikwame kwa sababu ya kukosa huduma. Tuna matarajio mengi kama nchi ikiwemo kunufaika na vipato vitakavyotokana na uwepo wa gesi na madini katika nchi yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...