Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akikabidhi zawadi ya simu ya kisasa ya I Phone 6 kwaajili ya kuboresha ufanisi kwa Ofisa Mwandamizi Uendelezaji Biashara Fatima Rajabu ambaye aliibuka mshindi wa jumla wa maigizo ya vitendo kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha. Kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba (NHC), David Shambwe akitoa mada kwenye kongamano hilo. Shambwe alizungumzia hatua muhimu za kuibua miradi kuitekeleza na hatimaye kuiuza kwa ufanisi kwa wateja na kufuatilia malipo baada ya kuuza nyumba zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...