Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii 

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeanzisha huduma ya bima ya afya kwa vikundi vya ujasiriamali,Shirika katika sekta binafsi ili kuweza kila mtanzania anapata huduma ya afya kupitia mfuko huo.

Akizungumza leo na wanavikundi vya ujasiriamali (ASSE),Meneja wa CHF- Makao Makuu ya NHIF,Costantine Makala amesema mfumo huo ni kikoa ambapo kila mmoja atachangia Sh.76,800 kwa mwaka.

Amesema kila mwana kikoa ambaye atalipa malipo hayo atatibiwa na bima ya afya mwaka mzima katika hospitali zote za serikali pamoja na baadhi ya hospitali binafsi.

Makala  amesema gharama za matibabu ni kubwa hivyo kila mjasiriamali anaweza kutumia fursa hiyo kwa kuchangia pamoja na wategemezi wake wasiozidi watano.

“Gharama za afya ni kubwa hivyo kila mmoja kutokana na gharama za uchangiaji anaweza kumudu katika mfumo wa kikundi na kupata matibabu yetote yanayolingana na mwanachama yeyote”alisema Makala.
Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Costantine Makala akizungumzia umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kwa vikundi vya wajasiliamali,katika mkutano uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Msimbazi Center,Ilala jijini Dar es salaam.wengine pichani toka kulia ni Mratibu wa Mtandao wa Mfuko wa Afya ya Jamii (TNCHF), Camillius Haul,Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) - Kanda ya Ilala,Christopher Mapunda pamoja na Afisa Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka Makao Makuu,Catherine Masingisa.
Mratibu wa Mtandao wa Afya ya Jamii,Kidani Magwira akitoa maelekezo ya namna ya kujaza fomu za ya kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya,katika mkutano uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Msimbazi Center,Ilala jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naomba mchanganuo bosi bima za afya kwa makundi mbalimbali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...