Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeanzisha huduma ya bima ya afya kwa vikundi vya ujasiriamali,Shirika katika sekta binafsi ili kuweza kila mtanzania anapata huduma ya afya kupitia mfuko huo.
Akizungumza leo na wanavikundi vya ujasiriamali (ASSE),Meneja wa CHF- Makao Makuu ya NHIF,Costantine Makala amesema mfumo huo ni kikoa ambapo kila mmoja atachangia Sh.76,800 kwa mwaka.
Amesema kila mwana kikoa ambaye atalipa malipo hayo atatibiwa na bima ya afya mwaka mzima katika hospitali zote za serikali pamoja na baadhi ya hospitali binafsi.
Makala amesema gharama za matibabu ni kubwa hivyo kila mjasiriamali anaweza kutumia fursa hiyo kwa kuchangia pamoja na wategemezi wake wasiozidi watano.
“Gharama za afya ni kubwa hivyo kila mmoja kutokana na gharama za uchangiaji anaweza kumudu katika mfumo wa kikundi na kupata matibabu yetote yanayolingana na mwanachama yeyote”alisema Makala.
Meneja
wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Costantine Makala akizungumzia umuhimu
wa kujiunga na bima ya afya kwa vikundi vya wajasiliamali,katika mkutano
uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Msimbazi Center,Ilala jijini Dar es
salaam.wengine pichani toka kulia ni Mratibu wa Mtandao wa Mfuko wa Afya ya Jamii (TNCHF), Camillius Haul,Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) - Kanda ya Ilala,Christopher Mapunda pamoja na Afisa Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka Makao Makuu,Catherine Masingisa.
Mratibu
wa Mtandao wa Afya ya Jamii,Kidani Magwira akitoa maelekezo ya namna ya
kujaza fomu za ya kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya,katika mkutano
uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Msimbazi Center,Ilala jijini Dar es
salaam.
Sehemu ya Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.
Naomba mchanganuo bosi bima za afya kwa makundi mbalimbali
ReplyDelete