wafungwa wa Kitanzania waliofungwa katika magereza ya Hong Kong.
Padri John Wotherspoon anayechapisha barua mbalimbali za wafungwa wa Kitanzania waliofungwa katika magereza ya Hong Kong baada ya kukamatwa na dawa za kulevya anafanya ziara nchini Tanzania kutembelea familia za wafungwa hao. Padri Wotherspoon alianza ziara yake mwishoni mwa mwaka jana na anaendelea na ziara ya kutembelea familia hizo hadi hivi sasa.
John Wotherspoon anasema aliwasili nchini akiwa na fedha za wafadhili kutoka Hong Kong kwa ajili ya kusaidia familia za wafungwa walio magerezani Hong Kong. Lakini fedha hizo zimeishia kwenye familia 5 tu huku bado akiwa na familia nyingine kama 30 za kutembelea na kuzijulia hali.
Padri huyo ambaye anayeendesha kampeni yake dhidi ya madawa ya kulevya kwenye tovuti yake ya Pope Francisamekuwa akichapisha barua nyingi kutoka kwa wafungwa wa Kitanzania walioko magerezani huko Hong Kong baada ya kukamatwa na dawa za kulevya. Barua hizo zinapatikana hapa ==>2013).
Mmhmm......
ReplyDeleteNina mpongeza huyu Padri kwa jitihada zake binafsi,kutembelea hizo familia. Napia kuwaona hao vijana walio magerezani huko China na Hongkong. Ukipitia hizo barua za hao vijana zimetaamka wazi njia zinazotumika,magwiji wa biashara hiyo hapa bongo.Lakini sijui kama serikali itachukua hatua yoyote kama sio kuunda tume itakayo angamiza kodi zetu bila mafanikio,. Kwa kifupi inasikitisha na ni dhambi kubwa kwa wale wanaotumia umasikini wa mtu mwingine kujinufaisha. Mhe JK chukua hatua kali tafadhali ushahidi uliopo unatosha. Nusuru vijana wetu.
ReplyDelete