Waziri
Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga (wa pili kutoka kulia) akizungumza jambo na
ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Ujumbe huo ulikwenda kumpa pole nyumbani kwake Bondo nje kidogo ya mji wa
Kisumu nchini Kenya kufuatia kifo cha mtoto wake Fidelis Castro Odhiambo Odinga
aliyefariki ghafla mapema mwezi huu.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akimfariji mama mzazi wa marehemu
Fidelis Castro Odhiambo Odinga
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akizungumza na wafiwa, Waziri Mkuu wa
zamani wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pamoja na Mkewe Mama Ida Odinga
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais wa zamani
wa Uganda Mama Miria Obote aliyehudhuria pia katika msiba huo Bondo nchini
Kenya.
Shabiki maarufu wa Timu ya Gor Mahia ya Kenya
akilia kwa uchungu katika ibada ya kumuombea marehemu Fidelis Castro Odhiambo
Odinga mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga aliyefariki
mwanzoni mwa mwaka huu.
Taaswira katika jukwaa kuu.
![]() |
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akihutubia maelfu ya Wakenya waliofika
katika viwanja vya Chuo Kikuu cha JOOUST
kwa ajili ya ibada ya Mazishi ya Fidel Odinga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...