Mwenyekiti
wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CCM,Ndugu Adam Kimbisa,wakati akitoka nje mara baada ya kumaliza kikao
cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa usiku huu,kilichofanyika leo
katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja,Zanzibar,kikao hicho kilianza mnamo majira ya saa sita mchana na kumalizika usiku mnamo saa mbili na ushehe hivi huku mambo mbalimbali yakiwa yamejadiliwa ikiwemo suala la sakata la Akaunti ya Escrow, hali ya kisiasa nchini, uchaguzi Mkuu na mambo ya Maadili na mengineyo.
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na
Wanahabari usiku wa kuamkia leo baada ya kikao cha kamati kuu cha CCM kuisha nje ya
ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Unguja kisiwani
Zanzibar.Nape ameeleza kuwa taarifa rasmi ya yaliyohusu kikao hicho atayaweka wazi asubuhi hii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...