Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho saa 11 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea leo Jumanne Januari 13, 2015 saa 9 alasiri maeneo ya Stesheni ya Pugu Mpiji ambapo mabehewa matatu ya treni ya mizigo iliyokuwa inasafiri kwenda Bara yaliacha njia na moja kuanguka kabisa.

Tayari Wahandisi wa TRL wako eneo la ajali kufanya tathmini na kuanza zoezi la uokoaji, ikiwemo kazi ya kuyanyanyua mabehewa yaliyopata ajali na kisha kukarabati njia ili iwezwe kupitika mapema hapo kesho.

Uongozi wa TRL inawaomba radhi wananchi na wateja wake wote nchini kwa usumbufu utakaojitokeza.


Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam,
Januari 13, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tanzania, kwa nini njia iko moja tu? kwa nini isijengwe njia ya pili kuepusha usumbufu kama huo? hii ni shiiiiiiiiiiida kweli mnapoteza mamilioni ya pesa kwa kitu kinachoweza kutekelezeka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...