Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhavile (kushoto) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), Dk Kitila Mkumbo wakikabidhiana nyaraka za makubaliano ya kuandaa midahalo kwa wagombea wa urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Katikati ni Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano, Dk Ayoub Rioba.
Picha na Venance Nestory.  



1. Katika nchi za kidemokrasia, midahalo ya wagombea imekuwa ni sehemu muhimu katika kufanikisha uchaguzi ulio huru, haki, wazi na amani. Midahalo hutoa fursa muhimu kwa wagombea kueleza falsafa, sera na mikakati yao ya kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi na nchi zao. Aidha, midahalo huwapa fursa ya kipekee wapiga kura na wananchi kwa ujumla katika kuwajua na kupima umahiri na weledi wagombea na vyama vyao. 
Kwa sababu hii, midahalo imekuwa ni sehemu muhimu ya uchaguzi katika nchi zinazoamini na kuzingatia misingi ya demokrasia. Tafiti zinaonyesha kuwa midahalo ya wagombea urais ina nafasi ya kipekee katika kuwawezesha wapiga kura kuamua mgombea gani wamchague na kwamba midahalo imekuwa ni chombo muhimu katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura kwa wingi. 

2. Kwa kuzingatia msingi ulioelezwa hapo juu, Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) na ITV/Radio One wamekubaliana kuandaa midahalo ya wagombea urais kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Tunaamini kwamba kwa kuandaa midahalo hii taasisi zetu hizi mbili zitakuwa zimetoa mchango muhimu wa kijamii katika kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka 20152 

3. Utaratibu wa jumla wa midahalo hii utakuwa kama ifuatavyo: 

a. Vyama vyote vitakavyoshiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na ambavyo vitasimamisha wagombea wa urais vitaalikwa kushiriki katika midahalo hii. 

b. Wagombea wote watakaojitokeza kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wataalikwa kushiriki katika midahalo hii. 

c. Midahalo itaanza kwa kushirikisha wagombea ndani ya vyama vyao pale ambapo chama kitakuwa na wagombea zaidi ya moja, na baadaye kati ya wagombea watakaokuwa wameteuliwa na vyama vyao. 

4. Utaratibu kamili wa midahalo hii utatolewa baadaye. 

5. Tunatoa wito na ombi maalumu kwa vyama vya siasa na wagombea wote watakaojitokeza kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kushiriki katika midahalo hii ili kuwapa wananchi fursa ya kuwajua; na wao kueleza falsafa, sera na mikakati yao na ya vyama vyao katika kukabiliana na matatizo yanayoikabili nchi yetu sasa na baadaye. 

Prof. Kitila Mkumbo

Mwenyekiti wa UDASA 

Joyce Mhavile 
Mkurugenzi Mtendaji ITV na RadioOne

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mmewauliza ccm kwanza kama mgomea wao atahudhuria hiyo midahalo? uzoefu wangu kwa chama hiki wanaweza kutafuta sababu waka timka kwa kuhofia kuumbuliwa hakikisheni mmekubaliana na ccm kwanza kwani nafahamu wapinzani hawana shida na uwazi watawala siku zote duniani ndio wenye mizengwe na wakipata fursa basi hujitowa.

    mdau.

    Mozambique.

    ReplyDelete
  2. Ombi, mtoe n'avais kwa watanzania walioko nje ya nichiez kuweza nao kudhitiki kikamilifu kushuhudia na kuweza kuwaulidza maswali hao wagombea live. Hiyo wekeni utaratibu wa internet streaming- in live for online viewers, na mruhusu maswali yaulizwayo online kuweza kujibiwa na wagombea.

    ReplyDelete
  3. Sisi kama wananchi mtupatie pia fursa ya kupendekeza maswali ya kuwauliza wagombea urais mtakapokuwa tayari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...