Tunasikitika kutangaza kifo cha ghafla cha  dada yetu mpendwa Leticia Mattei Rwechungura kilichotokea hapa Ujerumani tarehe 06.01.2015.Mazishi yatafanyika hapa Ujerumani Königswinter, karibu na mji wa Bonn tarehe 24.01.2015. Misa itaanza saa tano asubuhi (11:00 a.m.), katika Kanisa la St. Michael Niederdollendorf, Petersbergerstr. 14, 53639 Königswinter.

Dada Leticia Mattei alikuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko South Sudan (UNMIS) - United Nations Mission in Südan, Eastern Equatoria State of Torit-Sudan. Aliugua muda mfupi na kufariki dunia katika hospitali iliyoko mjini Bonn hapa Ujerumani. 

Watanzania wote walioko hapa Ujerumani, nyumbani Tanzania na ulimwenguni kote wameshtushwa na kifo hiki cha ghafla cha kuondokewa na mama yetu na dada yetu mpenzi Leticia Mattei. Tutamkumbuka daima kwa kazi kubwa alizoifanyia nchi yetu ya Tanzania, bara la Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Mungu amlaze mahali pema Peponi - Amin!
Kwa yeyote atakayependa kutoa sanda yake, tunaomba michango itumwe moja kwa moja kwa mtoto wa marehemu:

Diana Kajuna
IBAN: DE76 3806 0186 5501 3030 13
BIC: GENODED1BRS
Kreditinstitut: Volksbank Bonn Rhein-Sieg eG

Tunaomba sana ili tuweze kutekeleza mipango hii vizuri ya kumsindikiza dada yetu kwa heshima zote, wale wanaopenda kuhudhuria mazishi haya wawasiliane na mratibu wa shughuli hizi Nd. Majura, ili tupate orodha kamili ya wale wanaokuja ili itusaidie kuandaa mambo mengi ya muhimu. Kwa wale watakaopenda kupata malazi (ya hoteli), kadhalika tunaomba wawasiliane na Dr. Isack Majura kuanzia sasa kupitia:

Tel. +49 173 7089513
e-Mail: IMajura@aol.com
Germany

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. R.I.P. Dada Leticia.

    ReplyDelete
  2. R.I.P LETICIA ....GOD LOVED YOU MORE.
    MA SYMPATHY TO ALL FAMILY MEMBERS MAY GOD GUIDE YOU IN THIS DIFFICULT TIME.
    FROM MALONGOS FAMILY

    ReplyDelete
  3. R.I.P. Leticia,

    Although your work on earth is done
    Your life in heaven has just begun.
    Your struggles here were hard and long
    But they're over now, you're finally home.

    Life wasn't easy, by choice or fate
    A decision made, sometimes too late.
    A fight to the finish, always strong
    Rest easy Leticia, you're finally home.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...