Mkurugenzi wa Mradi wa Jengo la
Tatu la Abiria(Terminal III), Mhandisi Mohammed Milanga(mwenye suti), akiwaeleza
wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, namna ya mradi unavyoendelea, waliotembelea
Mradi huo leo asubuhi kuona maendeleo ya Ujenzi wake. Wa kwanza kushoto ni Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya
Uchukuzi,Bw. Biseko Chiganga na kushoto kwa Chiganga ni Afisa Usafirishaji,Bw.
Said Marusu.
Mkurugenzi wa Mradi wa Jengo la Tatu la Abiria
(Terminal III), Mhandisi Mohammed Milanga, akiwaeleza wataalam kutoka Wizara ya
Uchukuzi, utekelezaji wa ujenzi wa jengo hilo, waliotembelea sehemu unapotekelezwa
mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria leo asubuhi.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Hali ya Hewa Tanzania
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), John Mayunga, akiwapa maelezo wataalam kutoka
Wizara ya Uchukuzi juu ya namna Kompyuta maalum inayotoa taarifa za hali ya
inavyofanya kazi leo asubuhi, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho
kuona namna ambavyo Kituo hicho kinavyotoa taarifa kwa marubani na kwa sekta ya
usafiri wa Anga.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Hali ya Hewa Tanzania
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), John Mayunga, akiwapa maelezo wataalam kutoka
Wizara ya Uchukuzi juu ya namna Kompyuta zinazotumika kwa ajili ya utabiri wa
hali ya hewa zinavyofanya kazi leo asubuhi, wakati wataalam hao walipotembelea
kituo hicho. Wa kwanza kutoka kushoto ni
Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Said Marusu na wa
kutoka kulia ni Afisa Usafirishaji, Bw. Biseko Chiganga.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Hali
ya Hewa Tanzania katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere(JNIA), John Mayunga, akiwapa
maelezo wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi juu ya namna Mtambo wa kisasa wa
kuchambua data za hali ya hewa(computer cluster) inavyofanya kazi
leo asubuhi, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho kuona namna ambavyo
Kituo hicho kinavyotoa taarifa kwa marubani.
Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi
Ankal,
ReplyDeleteNimefurahi kuona kuwa wahusika wa mradi, kwa maana ya usimamizi na uhandisi, ni wananchi.
Miradi mkakati kama hii ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu itasaidia sana kuimarisha mawasiliano na kutupatia uwanja wenye hadhi utakaohudumia wasafiri wengi na mizigo mingi zaidi.
ReplyDelete