Meneja wa Kitengo cha taarifa za Usalama wa Usafiri wa Anga, Bw. Deodore Mushi akitoa maelezo ya namna ya mashine mbalimbali zinazotumika katika chumba maalum cha kutolea taarifa za usafiri wa Anga zinavyofanya kazi, kwa wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea katika ofisi hizo leo asubuhi kufanya tathimini ya utoaji wa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Wa Kwanza kulia ni Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Biseko Chiganga (aliyevaa koti jeusi), wa pili kushoto kwa Chiganga ni Afisa Usafirishaji, Bw Benjamin Mbimbi na tatu kutoka kushoto ni Afisa Usafirishaji, Bw. Said Marusu.
Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo, akifafanua jambo kwa wataalamu kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea kituo cha kuongozea ndege leo asubuhi kufanya tathmini ya utoaji wa huduma katika usafiri wa Anga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).
Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo akiwaonyesha wataalamu kutoka Wizara ya Uchukuzi, karatasi inayoonyesha aina ya ndege, mahali inapokwenda na muda itakaotumia inakokwenda, katika kituo cha uongozaji ndege kilichoko Katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere leo asubuhi wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho.
Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo (mwenye kilemba chekundu), akiwaelezaa wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, namna waongoza ndege wanavyotumia rada na kuelekeza marubani sehemu za kupita, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho leo asubuhi kufanya tathmini ya utoaji wa huduma katika usafiri wa anga katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. (Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...