Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, Soud Ahmed Al-Rahili akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii ,Dar

Watanzania wametakiwa kuonyesha ushirikiano katika sekta ya uwekezaji ili kuweza kuwavutia wawekezaji wa nje kuwekeza nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, Soud Ahmed Al-Rahili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati walipokuwa wakijadili masuala ya uwekezaji baina ya nchi ya Tanzania na Oman.

Al-Wahili amesema bidhaa za Tanzania zinazotarajiwa kupelekwa nchini Oman ni pamoja na nyama ya ng’ombe (Nyekundu) na Asali.Vitu hivyo vimekuwa na fursa katika soko la Oman hali ambayo watanzania waongeze juhudi ya kuzalisha kutokana na soko hilo kuwa pana na Tanzania ni nchi pekee inayoweza kunufaika na soko hilo.

Aidha  amesema  sekta ya uwekezaji ni pana kati ya Oman na Tanzania na ni wakati mwafaka kutumia fursa ya uwekezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...