Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Michael Mwande akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzungumzia mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 94.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC),James Andilile akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzungumzia mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 94. wengine pichani ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Michael Mwande (katikati) na Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO,Kapwalya Mhisomba (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wizi mtu uliondelea katika hii project. Mfano rahisi tuu wa compare ni bomba la gesi la 42 inch la Fayetteville Express lenye urefu wa 185 miles na wenye uwezo wa ku transport 1.2 Billion cubic feet a day umegharimu USD1.01 Billion. sasa vipi mradi wa songosongo wenye urefu wa 128.624miles na bomba la 16Inch utumie USD 1.225.

    ReplyDelete
  2. We mchangiaji wa kwanza wizi unatoka wapi? Hilo unaloongelea limejengwa lini? Mazingira ya ujenzi yanafafana? Mkandarasi anayejenga ndo huyo huyo? kuna vitu vingi vya ku vya kuangalia kabla hujatoa gharama zako!!

    ReplyDelete
  3. Mchangiaji wa kwanza kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla ya kuamua kulinganisha gharama! hilo unalosema limejengwa wapi? lini? Je mazingira ya ujenzi yanafanana? kama hayafanani ni wazi gharama hazitafanana! Mkandarasi ni huyo huyo? au mwingine? kama ni huyo huyo ndo ujiulize lkn kama sio utalinganishaje? yamejengwa wakati mmoja?? Sio kila cha wanasiasa kizuri jamani! Cha msingi kwanza hebu tusubiri gesi hiyo! Kila kukicha porojo za kutafuta umaarufu!

    ReplyDelete
  4. tatizo letu kila mtu anajiona mjuaji ,na wengi wetu wanaongea maneno ya kusikia kutoka kwa wanasiasa. Kitaalamu kuna factors nyingi zinazopanga bei,buyers bargaining power,suppliers bargaining power,terms of payment,number of competitors nakadhalika, sisi tunaskiliza maneno ya akina Zito ambao hutumika na mabalozi wa ulaya once wakikosa tenda ya makampuni yao.
    Kuna mambo mengi yametokea mpaka Tz inafanikisha mradi huu,Songas na Globeleq ambao ni waingereza walikuwa wanataka wamiliki mradi wote,Serikali ikajaribu kuomba fund(mkopo) kutoka Uk na Us bila mafanikio.waliweka masharti magumu ikiwemo kuruhusu makampuni binafsi kumiliki mradi huu kama ilivyo kwa Bomba la songosongo. Badala yake China wakakubali kutoa mkopo kupitia Exim Bank china,kuleta materials na wataalamu. Hii ndio sababu ya maneno mengi ya malalamiko na kejeli. Tuwe waangalifu ,tujue timu tunayoishangilia, na kwa maslahi ya nani.tusipoangalia tutajikuta tunatumika bila ya kujijua kwa maslahi ya wengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...