Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu, katika picha ya pamoja , Desemba 31, 2014 na baadhi ya wazee wasiojiweza wa Kambi ya Funga Funga iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu, akimkabidhi zawadi ya vyakula na mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya 2015 kwa Wazee wasiojiweza wa Kambi ya Funga Funga iliyopo Manispaa ya Morogoro, mnamo Desemba 31, 2014, zawadi hiyo ilipokelewa na Mwenyekiti wao Joseph Kaniki.
( Picha na John Nditi).
Na John Nditi, Morogoro
VIJANA wa chama cha Mapinduzi UVCCM wameshauriwa kujenga tabia ya kusaidi wazee wasiojiweza, kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwa lengo la kuwapa faraja badala ya kuachia jukumu hilo kwa serikali pekee kama ilivyo sasa.
Kauli hiyo ilitolewa Desemba 31, 2014 na Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu,wakati alipotembelea kituo cha kuwatunza wazee wasiojiweza cha Fungafunga cha Kichangani Manispaa ya Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...