Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Jumla ya watoto 63 wamezaliwa katika mkesha wa mwaka mpya 2015 katika hospitali za Temeke,Kinondoni pamoja na Ilala jijini Dar es Salaam.
Hospitali ya Temeke wamezaliawa watoto 19,Muuguzi wa zamu ,Rolester Kinunda alisema watoto 10 ni wakiume na tisa (9) ni wa kike na wazazi wa watoto hao wamejifungua salama na wameshapewa ruhusa .
Hospitali ya Amana Ilala watoto 21 wamezaliwa 11 wakiwa ni watoto wa kike na wakiume 10 na mapacha moja na kati ya watoto hao 21 wawili walifariki dunia.
Katika hospitali ya Mwananyamala iliopo kwenye Wilaya ya Kinondoni watoto 23 ambao kati yao watoto nane (8) ni wa kike na 15 ni wakiume ambapo wazazi pamoja na watoto waliruhusiwa.
Wauguzi katika Hospitali zote walitueleza kuwa watoto wote wamezaliwa wakiwa na afya bora na hakuna mtoto aliyezaliswa kabla ya siku zake (Njiti)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...